Monday, 22 February 2016

Felipe Anderson kusajiliwa Man United leo Feb 22 kwa euro milioni 60, huu ndio ukweli

February 22 vyombo kadha vya habari viliripoti kwa kuandika  stori kuwa klabu ya Man United imefanya usajili wa kiungo mshambuliaji wa Lazio  Felipe Anderson. Taarifa hiyo ambayo imeenea kwa kiasi kikubwa katika mitandao ya kijamii inaeleza kuwa Man United na Lazio wamekubaliana kila kitu kuhusu usajili wa kiungo huyo na kuwa anasubiri kujiunga na Man United mwisho wa msimu.
Felipe Anderson aliripotiwa kuwa usajili wake wa kujiunga na Man United mwishoni wa msimu umekamilishwa kwa dau la euro milioni 60, stori zilianza kuandikwa zaidi mchana wa February 22, lakini jioni ya February 22 Rais wa klabu ya Lazio Claudio Lotito amekanusha stori hizo na kuwa hakuna makubaliano yoyote yaliofanyika kati ya Man United na Lazio.
LAZIO SAMPDORIA 2014/2015 All'Olimpico ore 20,45 la LAZIO di Stefano PIOPLI affronta la Sampdoria di Sinisha MIHAJLOVIC anticipo serale della sedicesima giornata del Campionato di Serie "A" 2014/2015 ANDERSON (fotoTedeschi)
Kiungo wa kimataifa wa Brazil Felipe Anderson ambae ndio alikuwa anatajwa kuwa atajiunga na Man United mwishoni mwa msimu, aliwahi kutamba na klabu ya Santos kabla ya kutua Lazio ya Italia mwaka 2013 na amecheza zaidi ya mechi 60 akiwa na klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment