Ambwene Yessaya ‘AY’ amethibitisha kupokea taarifa ya kufungiwa kwa video ya wimbo ‘ Zigo remix’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz.
Akizungumza
na 225 katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, Jumatatu hii, AY amesema
alipokea barua yenye amri hiyo kutoka kwa rafiki yake ambae anafanya
kazi katika chombo kimoja cha habari.
“Sijaelewa
maadili gani kwa sababu kama maadili niliyokosea mimi ni kushoot kwenye
swimming pool, na kama kwenye swimmig pool watu nimevalisha jeans au
maturubai hapo nitakuwa nimekosa maadili,” alisema AY.
“Mavazi
ya kwenye swimming pool yako kila mahali, hata kwenye taarifa za habari
(Michezo) wanaonyesha waogeleaji, kama hiyo pia ni kukiuka maadili ni
sawa. Inashangaza mamlaka zetu wanafocus kwenye kufungia nyimbo zetu na
kuacha video za nje. Sijawahi sikia muziki wa Kenya, Uganda au Marekani
umefungiwa, kama wanaona nyimbo za Nicki Minaj zina maadili halafu Zigo
ya AY haina maadili baasi unaacha tu iwe hivyo ,” aliongeza AY.
Pia AY alisema barua hiyo ilitoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) ikisema kwamba video hiyo inakiuka maadili.
Kwa
mujibu wa Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungi, amethibitisha
kuvitumia vituo vya luninga nchini taarifa ya namna ya kupembua kazi za
wasanii zisizo na maadili.
No comments:
Post a Comment