Tuesday, 23 February 2016

Sokwe Ajifungua Kwa Upasuaji

Sokwe amezalishwa kwa upasuaji wa dharura kusini Magharibi mwa Uingereza katika sehemu uliyotengwa kwa kuhifadhia wanyama inayojulikana kama Bristol Zoo.

Mama na mtoto wa sokwe huyo wanaendelea vyema ,sokwe huyo alizaliwa kupitia upasuaji usio wa kawaida baada ya mama yake kuonyesha ishara za ugonjwa hatari wa shinikizo la damu.
Jopo la kuongoza shughuli ya upasuaji kwa sokwe huyo liliongozwa na Profesa David Cahill aliyeitwa kutoka hospitali ya kina mama NHS na mtoto wa kike alizaliwa kwa oparesheni hiyo.

Kumekuwa na sokwe wachache waliofanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua duniani,kisa cha hivi karibuni kikiwa kile cha San Diego Safari Park mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment