MKAZI
wa Mafinga, David Isack ( 32) alivamiwa na majambazi na kuporwa
sh.milioni 12 ambazo alikuwa akipeleka katika Benki ya DTB, ambapo
alivamiwa na watu watano wanatuhumiwa kuwa ni majambazi wakiwa na
usafiri wa pikipiki mbili aina ya boxer.
Akizungumza
na waandishi wa habari ijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro amesema kuwa tukio hilo
lilitokea Februari 12 mwaka huu katika eneo la Uwanja Ndege , katika
kurupushani za kutaka kuchukua fedha hizo walitokea askari na
kuwazingira na kisha kuanza kukimbia na kuweza kudondosha bunduki aina
ya SMG pamoja na risasi 24 ambazo zilitakiwa kutumika katika tukio hilo.
Amesema
askari walipowakamata wananchi walikusanyika katika tukio hilo na
kuanza kuwapiga watu wanaodaiwa kuwa majambazi mpaka kupoteza maisha
kutokana kushambuliwa huko na wengine watatu waliweza kukimbia na kiasi
hicho cha fedha.
Kamishna
Sirro amesema Isac alikuwa akitokea benki ya NMB na kwenda kupeleka
fedha hizo katika benki ya DTB iliyopo Quality Plaza.
Katika
operesheni nyingine imefanikiwa kukamata bastola moja ambayo
ilipatikana Februari 19 mwaka huu maeneo ya Kiwalani Kwa Gude kutokana
na polisi kupata taarifa juu ya watu kujificha katika kichaka kwa ajili
ya kufanya uhalifu na baada ya kugundua polisi wapo eneo hilo
walikimbia na kuacha silaha hiyo na jeshi la polisi linafanyia kazi
mmiliki wa silaha.
Hata
hivyo Jedhi la Polisi Kanda Maalumu linawashikilia watu wane wanaodaiwa
kuwa ni majambazi sugu waliowakamata eneo la Buguruni kwa Mnyamani
ambao ni Mohamed Hassan maarufu kwa jina Kidali (21)Mkazi wa Vingunguti
Speco,Hamis Alli (20) Mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani, Adam Salum (23)
Mkazi wa Buguruni kwa Madenge, Bakari Hamis (19) Mkazi wa Buguruni.
Aidha
amesema katika taarifa usalama Barabarani wameweza kukusanya zaidi ya
Sh. Bilioni moja iliyotokana na makosa ya magari kuanzia Januari 02
hadi Februari 22 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment