Umoja wa Mataifa
umeelezea hofu kuhusu hali ya taharuki iliyotanda nchini Uganda hususan
baada ya uchaguzi mkuu wa urais uliokamilika majuzi
Afisi ya haki
za kibinadamu ya Umoja huo inaelezea wasiwasi kufuatia kuwepo kwa hali
ya uhasama mkubwa baina ya rais wa jamhuri Yoweri Museveni na viongozi
wa upinzani akiwemo kanali mstaafu Kizza Besigye.Kuimeibuka taharuki kufuatia mauaji ya watu wawili na vilevile kamata kamata ya kiongozi wa upinzani daktari Kizza Besigye kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya urais.
Dakta Besigye amepinga matokeo ya uchaguzi akisema kuwa haukuwa wa haki na huru.
Katika taarifa yake Umoja wa mataifa unaelezea jinsi maafisa wa usalama wamekuwa wakitumia nguvu kupita kiasi wanapokabiliana na watu wasiokuwa na silaha ambao msimamo wao unaelekea upande wa chama cha upinzani FDC.
''Inatisha sana ukitizama shime ambayo polisi na jeshi la Uganda ilikuwa nayo ilipovamia afisi za chama cha FDC siku ya ijumaa '' taarifa hiyo inaelezea.
Juma lililopita waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani John Kerry alizungumza na rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa simu na kumwelezea wasiwasi wake kuhusiana na matumizi ya nguvu kupita kiasi wanaposhughulika na wafuasi wa upinzani.
Aidha Kerry alizungumzia swala la uhuru wa viongozi wa upinzani mbali na kujadili hatua ya serikali kufunga mitandao ya kijamii siku ya uchaguzi.
No comments:
Post a Comment