Nchi
ya Uingereza imempongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wa serikali
yake hususani katika kupambana na ubadhirifu wa mali za umma na ufisadi,
kwa siku chache alizokaa madarakani.
Sifa hizo za Uingereza zimewasilishwa jana Ikulu jijini Dar es Salaam na Balozi wa nchi hiyo,, Balozi Dianna Melrose.
Balozi
Melrose alieleza kuwa nchi yake imeridhishwa na juhudu za Rais Magufuli
katika kulinda fedha za umma na kuahidi kushirikiana naye hususan
katika kuimarisha idara ya Mahakama na Intelijensia nchini.
“Tunadhani
ameonesha msimamo mkali dhidi ya rushwa na ufisadi, na miongoni mwa
mambo ambayo tumezungumza ni namna ya kufanya kazi pamoja katika
kupambana na rushwa. Tuna mazungumzo katika kuimarisha mifumo ya
kiintelijensia na mahakama,” alisema Balozi Melrose.
Katika
hatua nyingine, Rais Magufuli alikutana na rais Mstaafu, Dk. Jakaya
Kikwete Ikulu lakini mazumgumzo kati yao hayakuwekwa wazi.
No comments:
Post a Comment