Wednesday, 20 January 2016
MESSI, SUAREZ NA NEYMAR WAFUNGIWE NA FIFA (,NI UTANI TU WA KOCHA NANI KASEMA SOMA)
Bosi wa timu ya taifa ya Chile Jorge Sampaoli ametania kuwa washambuliaji Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar wanatakiwa kufungiwa na shirikisho la mpira wa miguu duniani kwani umoja wao unaounda MSN ni hatari zaidi ya ule wa Real Madrid BBC. Kocha huyo aliyewapa ubingwa wa CONCACAF wa mataifa ya Amerika kusini Chile amesema akiwa katika utani kuwa FIFA wanatakiwa kuingilia suala hilo la MSN kwani umoja wao ni habari mbaya zaidi katika soka.
Akizungumzia ubora wa utatu huo wa Barcelona, Sampaoli ambaye alikua katika top 3 ya kuwania tuzo za FIFA za kocha bora wa dunia sambamba na Pep Guadiola na Luis Enrique, amesema kuwa Messi pekee anaweza kushinda mechi, sasa ukimuongezea Suarez na Neymar, ni hatari zaidi.
Sampaoli akielezea tofauti kati ya MSN na BBC amesema kuwa siri kubwa ya ubora wa MSN ni mahusiano yao (ushirikiano) kiuchezaji tofauti na BBC ambapo kocha huyo anasema kuwa kila mtu anacheza kivyake.
Aidha kocha huyo amewazungumzia makocha Pep Guadiola na Muargentina Marcelo Bielsa kama bora zaidi duniani kutokana na aina yao ya ufundishaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment