Wednesday, 20 January 2016

JE, HILI NDIYO PAMBANO LA MWISHO LA MANNY PACQUIAO?

Pacquiao

Bondia Mphilipino Manny Pacquiao amesema kuwa wakati umefika kwake kutundika gloves na kuacha ndondi ili apate muda mzuri wa kuisaidia jamii masikini kwao Uphilipino kwa kujihusisha moja kwa moja na siasa. Pacquiao atapigana pambano lake la mwisho mwezi April mwaka huu na bondia Anthony Bradley ambaye aliwahi kumpiga ManPac mwaka 2012 kabla ya Pacquiao kusawazisha mwaka 2014 na sasa wanataka kufunga kitabu.
Tayari bondia Manny Pacquiao ambaye hajapigana tangu apoteze pambano lake na Floyd Mayweather mwezi mei mwaka jana ni mbunge nchini kwao na anatarajia kutetea kiti cha useneta katika uchaguzi ujao wa nchini mwao.
Akiongea katika mkutano wa kupromote pambano lake la mwisho dhidi ya Bradley Los Angeles, ManPac amesema kuwa kitu kizuri katika maisha sio kujihudumia mwenyewe bali jamii na kusisitiza kuwa maisha ni mafupi mno, hivyo ni vizuri akaacha ngumi na kujikita katika kutoa huduma kwa jamii.
Pacquiao (37) ameendelea kusema kuwa ni huzuni kuacha ngumi, lakini hawezi kupigana maisha yote. Pambano hilo la mwisho la Pacquiao litafanyika MGM Arena.

No comments:

Post a Comment