Monday, 7 December 2015

WAFANYANYA BIASHARA NDOGO NDA IRINGA

mwekikiti wa jumuiya ya wafanya biashara mkoa wa iringa(JWT) bw Odilo Nyamlaga akifafanua jambo NA WAANDISHI WA HABARI HAPO JANA


 
Wafanya biashara ndogo ndogo alimaarufu kama wamachinga hapo jana walikumbwa na hali ya taharuki baada ya kupewa taarifa a kubomolewa kwa vibanda vyao pamoja na kusimamishwa kwa shughuli zao ndogo ndogo ambazo wanazifanya katika baadhi ya maeneeo ya nayo izunguka mji wa iringa  .

 Tukio hilo ambalo lilitokea mapema hapo jana kwa wafanya biashara hao wakiwa wamekusanyika pamoja katka maeneo ya gadeni ya Iringa kwaajili ya kusikilizia muhstakabari wao mzima juu ya shughul zao za ujasiriamali.

Ndipo baada ya kukaa kwa masaa kadhaa ndipo viongozi wao wa juu wa chama hiko walitoka katika kikao kilichokuwa kikifayika kwa mkurugenzi wa mkoa wa iringa na kuwapa mrejesho mzima wa yale yaliyotkana na kikao hiko.

Akiongea na wafanya bishara hao mwenyekiti wawafanyabiashara ndugu odillo alitoa baadhi ya mabo ambayo yameidhinishwa na mkurugenzi ,.

1.Wafanyabiashara wote wanaofanya biashara mahahali mabapo sisalama kwa walaji basi lazima atafute sehemu nzuri.

2.Waafanya biashara wa vyakyula almaarufukama mama ntilie wanatakiwa kutoweka vyakula CHINI .

3.Wafanyabiashara ndogo ndogo wote wanao fanya biashara pembezoni mwa barabara pia wanatakiwakujipanga ndani ya siku saba walizopewa na mkurugenzi wa mkoa.

4.Halmashauri ya Irnga imewaongezea siku 7 kwa wajasiriamali wadogo wadogo wote ili waweze kuimarsha maeneo yao ya biashara.


Hata hivyo pia  kwa upande mwingine Ndugu Odillo amewasihi wafanya biashara wadogoo wadogo kutumia nafasi hiyo kujiunga na jumuiya ya wafanya bishara ndogo ndogo ili waweze kutambuliwa na kutambulika na jumuiya hiyo ya wafanya biashara,kwani kuna tija kubwa kwao kama wajasiliamari.

Kwaupande wake Mwenyekiti wawafanya biashara ndogo ndogo mkoa wa Iringa amesema kuwa wao kama jumuiya ya wafanyabiashra ndogo ndogo  wamepokea kauli hiyo ya Mkurugenzi wa mkoa na kusema kuwa wapo tayari kuyafuata ,lakini serikali inapswa kuwafikiria kwa upande wapili kwa namna nyingine kwani wao ndiyo wapo wengi na wengi wao wamekuwa wakitumia biashara hizo hizo kusomesha watoto,kuhudumia familia zao na kujikimu na umaskini .



No comments:

Post a Comment