Saturday, 5 December 2015

CECAFA CHALENJI CUP 2015: UGANDA MABINGWA TENA KWA MARA YA 14!

Image result for cecafaLEO huko Addis Ababa Nchini Ethiopia, Uganda imetwaa Kombe la Chalenji Cup baada ya kuifunga Rwanda 1-0 na kutwaa Kombe na Tuzo ya Dola 30,000.
Ushindi huu wa Uganda, maarufu kama The Cranes, umewapa Taji lao la 14 la Ubingwa wa Nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Bao lao la ushindi lilifungwa na Ceasar Okhuti katika Dakika ya 15 alipounganisha kwa Kichwa Krosi ya Fulbeki wa Kulia Denis Okot.
Kabla ya Fainali hii ilichezwa Mechi ya kusaka Mshindi wa 3 kati ya Ethiopia na Sudan na Wenyeji Ethiopia kushinda kwa Mikwaju ya Penati 4-3 baada ya Sare ya 1-1.

No comments:

Post a Comment