LIGI KUU ENGLAND
Stoke 2 Man City 0
Arsenal 3 Sunderland 1
Man United 0 West Ham 0
Southampton 1 Aston Villa 1
Swansea 0 Leicester 3
Watford 2 Norwich 0
West Brom 1 Tottenham 1
2030 Chelsea v Bournemouth
LEICESTER CITY wamepaa kileleni mwa Ligi Kuu England baada ya kuichapa Swansea City Bao 3-0 kwa Hetitriki ya Riyad Mahrez.
Arsenal, ambao waliishinda Sunderland 3-1, wakishika Nafasi ya Pili huku waliokuwa Vinara City wakishuka hadi Nafasi ya 3 baada kuchapwa 2-0 na Stoke City na Man United kwenda
Nafasi ya 4 baada kutoka 0-0 na West Ham.Bao za Arsenal zilifungwa na Joel Campbell, Olivier Giroud, ambae pia alijifunga mwenyewe na kuipa Sunnderland Bao lao, na la 3 kupigwa na Aaron Ramsey.
Baada ya Matokeo haya ya Leo kwa Timu za juu, Leicester sasa ni Vinara wakiwa na Pointi 32 wakifuatiwa na Arsenal wenye Pointi 30 na kisha Man City na Man United zenye Pointi 29 kila mmoja.
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumapili Desemba 6
1900 Newcastle v Liverpool
Jumatatu Desemba 7
2300 Everton v Crystal Palace

No comments:
Post a Comment