Usiku wa December 2 ilikuwa ni zamu ya
kuchezwa kwa mechi za Copa del Rey nchini Hispania, michezo nane
ilichezwa usiku wa December 2 ila mchezo uliyochezwa mapema zaidi ni
mchezo kati ya FC Barcelona dhidi ya Villanovense uliyopigwa katika
dimmba la Nou Cam
Kwa sasa FC Barcelona unaweza kuita ndio
timu inayoongoza kwa safu bora ya ushambuliaji kutokana na ushindi wa
mechi zao za hivi karibuni kuibuka na ushindi wa idadi kubwa ya magoli,
matokeo ya mechi zao nne zilizopita zinaonesha kuwa walimfunga Real
Madrid 4-0 LALIGA, wakamfunga AS Roma 6-1 UEFA, wakamfunga Real Sociedad
4-0 na usiku wa December 2 wameifunga Villanovense goli 6-1 katika
mchezo wa Copa del Rey.
Kwa takwimu hizo FC Barcelona wanakuwa
wamefunga jumla ya 20 ndani ya mechi nne ambapo ni wastani wa goli 5 kwa
kila mechi, magoli ya FC Barcelona yamefungwa na Daniel Alves dakika ya
4, Sandro Ramirez dakika ya 21, 31, 69 na Munir El Haddadi dakika ya 51 na 76 wakati goli pekee la Villanovense lilifungwa na Juanfran dakika ya 29.



No comments:
Post a Comment