Monday, 26 October 2015

VAN GAAL : NIMECHOKA MASWALI KUHUSU KIWANGO CHA ROONEY


ROONEY-30Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesema yupo ‘taabani’ na maswali kuhusu kiwango cha Kepteni wake Wayne Rooney baada ya Mchezaji huyo kudorora wakati wa Dabi ya Manchester iliyoisha 0-0.

Rooney, ambae ndie Nahodha wa Man United, amefunga Bao 2 kwenye Mechi 9 za Ligi Kuu Msimu huu na kwenye Mechi ya Jumapili na Man City Uwanjani Old Trafford hakuonekana kabisa kiasi cha Wanahabari kuhoji kwanini Van Gaal anaendelea kumkumbatia Straika huyo wa Umri wa Miaka 30.

Kwenye Mechi hiyo na City, Rooney alichezeshwa kama Straika pekee mbele na alimudu Shuti moja tu, ambalo halikulenga Goli, na mara pekee aliyogusa Mpira kwenye Boksi la City ni katika Dakika ya 70.

Lakini Van Gaal alipotajwa Rooney tu kwenye Mahojiano baada ya Dabi hiyo hapo Jana alivimba na kujibu: “Hivi ni lazima niongee kuhusu Rooney kila Wiki? Kwa nini?”
Aliongeza: “Nyie mna mawazo yenu, andikeni tu. Sitoi jibu lolote kuhusu Rooney. Nachefuliwa na maswali hayo!”

No comments:

Post a Comment