Kipa
wa Chelsea, Asmir Begovic akiruka bila mafanikio kuzuia mpira wa kichwa
wa Andy Carroll, uliopa bao la ushindi West Ham nyumbani dakika ya 79
Uwanja wa Upton Park katika
mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo. West Ham maarufu 'Wagonga
Nyundo' wameshinda 2-1, bao lao lingine likifungwa na Mauro Zarate dakika ya 17, huku la Chelsea iliyompoteza Nemanja Matic aliyeonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 44 Gary Cahill dakika ya 56. Makocha Jose Mourinho wa Chelsea na Silvino Louro pia walitolewa uwanjani
No comments:
Post a Comment