Zipo ripoti zimezagaa huko England kuwa Meneja wa Chelsea Jose Mourinho atafukuzwa kazi ikiwa Timu yake itafungwa na Liverpool kwenye Ligi Kuu England.
Ripoti hizo zimedai Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich,
ameghadhibika baada kuiona Timu yake ikichapwa 2-1 huko Upton Park na
West Ham hapo Jumamosi Siku ambayo ilikuwa ni Sherehe ya Bethdei yake.
Kipigo hicho cha Mechi hiyo kimewatupa Chelsea, ambao ni Mabingwa
Watetezi, Nafasi ya 15 kwenye Ligi Kuu England wakiwa Pointi 11 nyuma ya
Vinara Man City baada ya Mechi 10 kuchezwa.
Juu ya kipigo hicho, kwenye Mechi hiyo, Mourinho, Msaidizi wake
Silvino Loura na Mchezaji wake Nemanja Matic wote walitolewa nje kwa
Kadi Nyekundu.
Jumanne Chelsea, ambao pia ni Mabingwa Watetezi wa Capital One Cup,
wapo Ugenini kuchezi Mechi ya Raundi ya 4 ya Kombe hilo na Timu
isiyotabirika Stoke City.
Lakini Mechi inayodaiwa ndio itamfukuzisha kazi Mourinho ni ile ya
Ligi ya Jumamosi dhidi ya Liverpool ambayo sasa iko chini ya Mjerumani
Jurgen Klopp.
Klopp, alipokuwa Borussia Dortmund Mwaka 2013, aliwahi kuitwanga
Real Madrid chini ya Mourinho Bao 4-3 kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI.
No comments:
Post a Comment