Tuesday, 23 August 2016

MAZEMBE YAICHAPA YANGA 3-1 NA KUONGOZA KUNDI A

DSC_0647


Mchezo wa mwisho wa Kundi A michuano ya kombe la Shirikisho Afrika kati ya TP Mazembe dhidi ya Yanga umemalizika kwa Yanga kukubali kichapo cha magoli 3-1 ikiwa ugenini na kuendeleza rekodi yake ya kutoshinda michezo yake mitatu ya hatua ya nane bora msimu huu.


Bolingi alianza kuifungia Mazembe bao la kwanza dakika ya 28 kipindi cha kwanza.
DSC_0657 (1)
Yanga ilipata pigo dakika mbili baada ya kuruhusu goli, Andrew Vicent ‘Dante’ alioneshwa kadi nyekundu na kuiacha Yanga ikicheza pungufu kwa dakika zote zilizobaki.
DSC_0632
Dakika 11 baada ya kipindi cha pili kuanza, Rainford Kalaba aliifungia Mazembe bao la pili kabla kuongeza bao lake la pili likiwa ni bao la tatu kwa Mazembe mnamo dakika ya 64.
Amis Tambe aliifungia Yanga bao pekee akiunganisha mpira uliogonga ‘mtambaa panya’ baada ya Haruna Niyonzima kupiga mpira wa adhabu ndogo.
DSC_0645
Matokeo hayo yanaipa Mazembe fursa ya kuongoza Kundi A kwa pointi 13 ikifatiwa na Medeama yenye pointi 8 licha ya kupoteza mcheza wake wa mwisho ugenini dhidi ya MO Bejaia. Bejaia imemaliza katika nafasi ya tatu ikilingana kwa pointi na Medeama lakini haijafanikiwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali.
IMG-20160823-WA0008 (2)
Yanga  imemaliza ikiwa nafasi ya nne (yamwisho) kwenye Kundi A ikiwa na pointi nne baada ya kupata ushindi katika mechi moja (Yanga 1-0 MO Bejaia) sare moja (Yanga 1-1 Medeama) huku mechi nyingine nne ikiwa imepoteza. (MO Bejaia 1-0 Yanga, Yanga 0-1 TP Mazembe, Medeama 3-1 Yanga, Mazembe 3-1 Yanga).
DSC_0691
Yanga imefungwa jumla ya magoli 9 huku yenyewe ikiwa imefunga magoli manne katika mechi zote 6 ilizocheza.
Kwahiyo, TP Mazembe na Medeama zinafuzu hatua ya nusu fainali ya kombe ka shirikisho Afrika na kuziacha MO Bejaia na Yanga kutoka Kundi A.
Group A
DSC_0689

No comments:

Post a Comment