Monday, 11 July 2016

REKODI ALIZOVUNJA RONALDO KWENYE EURO

Ronalro-record breking



Licha ya kutolewa nje mapema kwenye mchezo wa fainali, lakini nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo ameongeza kitu kingine kwenye maisha yake ya soka.
Akicheza kwa mara ya nne kwenye michuano ya Ulaya, mwisho wa siku nyota huyo mwenye miaka 31 alinyanyua ndoo kutokana na ushindi wa kikosi wa bao 1-0 katika dakika za nyongeza kwenye dimba la Stade de France dhidi ya wenyeji Ufaransa. Ilikuwa ni kumbukumbu nyingine kwa star huyo wa Real Madrid ambaye amekuwa akifanya vizuri kwenye  michuano ya Ulaya tangu alipoanza kucheza kwa mara ya kwanza mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 19.
Mfungaji mwenye magoli mengi kwenye fainali za Euro
Ameweza kuifikia rekodi ya mfungaji wa muda wote Michel Platini kwa kufunga magoli matatu katika fainali za mwaka huu baada ya kufunga goli kwa kichwa kwenye mechi dhidi ya Wales.
9: Cristiano Ronaldo (Portugal), Michel Platini (France)
7: Alan Shearer (England)
6: Ruud van Nistelrooy (Netherlands), Patrick Kluivert (Netherlands), Wayne Rooney (England), Thierry Henry (France), Nuno Gomes (Portugal), Zlatan Ibrahimović (Sweden), Antoine Griezmann (France)
Mchezaji aliyecheza fainali nyingi za Euro
Ronaldo alisafiri kuelekea Ufaransa akiwa ameshacheza mechi 14 katika fainali mbalimbali zilizopita. Siku chache baadaye akaivunja rekodi ya golikipa wa Uholanzi Edwin van der Sar na beki wa Ufaransa Lilian Thuram ya kucheza mechi 17 kwenye sare ya magoli 3-3 dhidi ya Hungary. Akianza kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Ufaransa sasa ameweka rekodi ya kucheza mechi 21 kwenye michuano hiyo.
21: Cristiano Ronaldo (Portugal)
18: Bastian Schweinsteiger (Germany)
17: Gianluigi Buffon (Italy)
16: Lilian Thuram (France), Edwin van der Sar (Netherlands), Cesc Fàbregas (Spain), Andrés Iniesta (Spain)
15: Sergio Ramos (Spain), David Silva (Spain)  
Mchezaji aliyecheza mechi nyingi kwenye timu ya taifa ya Ureno.
Licha ya kwamba alikosa mkwaju wa penati kwenye mchezo kati ya Ureno dhidi ya Austria, mchezaji huyo wa zamani wa Sporting CP na Manchester United amevunja rekodi ya star mwingine wa Ureno Luis Figo ya kucheza mechi nyingi kwenye kikosi cha Ureno kwa kufikisha mechi 128.
133: Cristiano Ronaldo (2003–)
127: Luís Figo (1991–2006)
110: Fernando Couto (1990–2004)
103: Nani (2006–)
94: Rui Costa (1993–2004)
Mchezaji wa kwanza kufunga kwenye Euro nne tofauti
Ronaldo alianza michuano ya Euro 2016 akiwa miongoni mwa wachezaji saba ambao wameshafunga katika mara tatu katika Euro tatu tofauti na alikuwa akipambana na Zlatan Ibrahimović kuwa mchezaji wa kwanza kuweka rekodi ya kufunga kwa mara ya nne katika Euro nne tofauti.
Alisubiri hadi mechi ya tatu kuweza kukamilisha hilo katika michuano iliyomalizika nchini Ufaransa lakini mpinzani wake msweden Zlatan hakuweza kufumania nyavu. Ronaldo aliweka rekodi hiyo baada ya kupiga bao mbili kwenye mechi dhidi ya Hungary. Alipofunga goli kwenye mchezo dhidi ya Wales akawa mchezaji wa kwanza kufunga magoli matatu katika fainali tofauti za Euro.
Magoli ya Ronaldo kwenye michuano ya Euro
2004 v Greece (1), Netherlands (1)
2008 v Czech Republic (1)
2012 v Netherlands (2), Czech Republic (1)
2016 v Hungary (2), Wales (1)
Mfungaji bora wa muda wote wa Euro (mechi za kuwania kufuzu zimehesabiwa)
Nyota huyo wa Ureno anamuongoza Ibrahimović kwenye orodha ya mfungaji wa muda wote kwenye michuano ya Euro ukichukua magoli yake tisa aliyofunga kwenye fainali za michuano hiyo ukijumlisha na magoli mengine 20 aliyofunga kwenye mechi za kuwania kufuzu, matano kati ya hayo amefunga wakati wa kuwania kufuzu kucheza fainali za mwaka huu zilizofanyika Ufaransa na kuwa na jumla ya magoli 29.
29: Cristiano Ronaldo (Portugal)
25: Zlatan Ibrahimović (Sweden)
23: Robbie Keane (Republic of Ireland)
22: Hakan Şükür (Turkey), Jon Dahl Tomasson (Denmark)
21: Jan Koller (Czech Republic)
Kwa upande mwingine, rekodi mbili za Ronaldo zilivunjwa kwenye michuano iliyomalizika…
Mchezaji mwenye umri mdogo kucheza fainali ya Euro
Fainali ya Jumapili ilikuwa ni ya pili kwa Ronaldo baada ya kuandika historia kwenye fainali yake ya kwanza ya Euro mwaka 2004.
Mechi hiyo ya mwaka 2004 ilimalizika kwa Ureno kufungwa na Ugiriki lakini Ronaldo aliacha alama ya kuwa mchezaji mwenye miaka 19 na siku 150 kucheza fainali ya Euro rekodi ambayo ilidumu hadi ilipovunjwa na Renato Sanchez aliyeanza kwenye kikosi cha Ureno kilichocheza fainali dhidi ya Ufaransa akiwa na miaka 18 na siku 328.
Ronaldo pia alikuwa mchezaji mdogo kwenye michuano mikubwa alipokuwa kwenye kikosi cha Ureno kilichoshiriki fainali za Euro mwaka 2004 na kufunga goli kwenye mchezo waliochapwa 2-1 na Ugiriki kwenye mchezo wa ufunguzi akiwa na miaka 19 na siku 128. Renato Sanches akajaingia akitoka benchi kwenye mchezo wa kwanza kwenye fainali za mwaka huu akiwa na miaka 18 na siku 301 na kuvunja rekodi ya Ronaldo kwenye mechi waliyobanwa na kulazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Iceland.
Rekodi nyingine zinazoshikiliwa na Cristiano Ronaldo
Timu ya taifa (Ureno)
  • Mchezaji aliyecheza mechi nyingi kwenye michuano ya Euro: 21
  • Mchezaji mwenye magoli mengi kwenye fainali za Euro: magoli 9 (sawa na Michel Platini)
  • Mchezaji aliyefunga kwenye michuano mingi ya Euro: Euro 4
  • Mchezaji pekee kufunga magoli matatu kwenye fainali mbili za Euro
  • Magoli mengi kwenye michuano ya Euro ukijumlisha na ya kuwania kufuzu: magoli 29
  • Mechi nyingi kwenye kikosi cha Ureno: 21
  • Mfungaji mwenye magoli mwengi kwenye timu ya Ureno: 61
Klabu
  • Magoli mengi kwenye michuano ya UEFA Champions League: 93
  • Magoli mengi kwenye klabu ya Real Madrid : 364
  • Magoli mengi kwenye UEFA Champions League kwa msimu: 17 (2013/14)
  • Tuzo ya ESM Golden Shoe: 4 (2007/08, 2010/11, 2013/14, 2014/15)
  • Mchezji aliyechaguliwa mara nyingi kwenye kikosi bora cha mwaka cha UEFA: 10 (2004, 2007–2015)

No comments:

Post a Comment