Rapper The Game aliitisha matembezi hayo kupitia Instagram yake na kusema wanaotakiwa kushiriki kwenye matembezi hayo ni Wanaume tu, Wanawake na watoto wabaki nyumbani na kwamba Mwanaume yeyote atakaekuja hatakiwi kuwa na silaha yoyote.
Ni matembezi yaliyokua na kusudi la kuondoa hofu baada ya mauaji kutokea na kuurudisha umoja na ushirikiano kati ya Polisi na Wananchi, kuanzisha uhusiano mpya na kuondoa hofu ya kuwindana baina ya Polisi na raia.
Kwenye hii movement yao iitwayo H.U.N.T (Hate Us Not Today) viongozi Snoop Dogg na The Game walikutana na uongozi wa Polisi pamoja na Meya wa Los Angeles Eric Garcetti.
The Game amesema ameguswa kufanya hivyo sababu ameona hali inavyoelekea ni kwamba Ubinaadamu unaondoka ndio maana akaamua kutumia ushawishi wake kusaidia kumaliza au kukiondoa kinachotaka kutokea, sisi sio Wanyama.
No comments:
Post a Comment