| Rais Barrack Obama wa Marekani amewasihi wamerakani wajizue dhidi ya hisia kali baada ya Mmarekani Mweusi kuwapiga risasi na kuwaua maafisa watatu wa polisi katika shambulizi la pili la kulipiza kisasi |
Rais Barrack Obama
wa Marekani amewasihi wamerakani wajizue dhidi ya hisia kali baada ya
Mmarekani Mweusi kuwapiga risasi na kuwaua maafisa watatu wa polisi
katika shambulizi la pili la kulipiza kisasi dhidi ya polisi wazungu
wanaowaua wamarekani weusi.
Obama ameomba uvumilivu utawale mioyo ya wakaazi wa mji wa Baton Rouge Louisiana nchini Marekani ambao sasa wanahofu ya kuzuka mashambulizi ya kulipiza kisasi.
| Gavin Long ambaye ni mwanajeshi wa zamani aliwapiga risasi polisi kulipiza kisasi mauaji ya Alton Sterling |
Alton Sterling pasi na hatia yeyote majuma mawili yaliyopita.
| Alton Sterling aliyeuawa na polisi mzungu pasi na kosa lolote |
Gavin Long ambaye ni mwanajeshi wa zamani alikuwa amerekodi ujumbe katika mji wa Dallas siku chache baada ya polisi watano kuuawa mjini humo katika shambulizi lililotekelezwa kulipiza kisasi cha mauaji ya Sterling.
Long mwenye umri wa miaka 29 aliwahi kuhudumu kama mwanajeshi wa Marekani .
Rais Obama ameshauri watu weusi dhidi ya kutekeleza mashambulizi dhidi ya Polisi akisema mauaji ya kulipiza kisasi sio suluhisho la tatizo sugu la ubaguzi wa rangi bali utachochea uhasama zaidi dhidi yao na polisoi wazungu.
No comments:
Post a Comment