Haya
ni mambo ya kawaida katika maisha kwani maisha ni wigo, lakini mwigo
wenye uhalisia wa kweli kulingana na mazingira, wakati, uwezo na
uthubutu wa mtu katika jambo analolifanya.
Tumekuwa tukisoma na hata kusikia mazungumzo ya kawaida na
kwenye vyombo vya habari juu ya ndoto za wajasiriamali. Baadhi yao
wamekuwa wakisema wanataka kuwa kama mfanyabiashara fulani maarufu
kutokana na biashara wanazozifanya.
Haya ni mambo ya
kawaida katika maisha kwani maisha ni wigo, lakini mwigo wenye uhalisia
wa kweli kulingana na mazingira, wakati, uwezo na uthubutu wa mtu katika
jambo analolifanya.
Katika kufanikisha yale ambayo
unayafanya na hata unayotaka kuyafanya kwa mafanikio katika shughuli
zako za ujasiriamali, huna budi kufanya mambo kadha wa kadha kama tabia
zako za kila siku za utendaji wako wa kazi.
Jaribu
kufikiria juu ya uwezo ulionao katika utendaji kazi wako kwani
wajasiriamali waliofanikiwa wanajua udhaifu wao na hawathubutu kuona
kama vitu vya kuwakwamisha katika shughuli zao, bali wanachukulia kama
moja ya fursa za kufikia malengo yao.
Wajasiriamali
waliofanikiwa hujaribu kutumia njia mpya kwa lengo la kuimarisha mbinu
za biashara zao kwa kuhakikisha hawafanyi upotevu wowote wa rasilimali
katika mchakato mzima wa uendelezaji na uendeshaji wa biashara zao.
Jaribu
kufikiria juu ya wateja wako kwani wateja ndiyo roho ya biashara yako.
Bila wao hakuna biashara, kwani hakuna familia yoyote hapa duniani
ambayo imewahi kuendesha biashara kwa kujitegemea kama wateja
wanaojitosheleza.
Jambo la msingi hapa ni kujua au
kupata taarifa za jumla ya idadi ya watu, hususani wateja ambao watakuwa
watumiaji wa bidhaa au huduma unazozitoa kwani ni muhimu kukumbuka kuwa
mchakato wa kutafuta soko au kujaribu kuuza bidhaa kwa watu ambao
hawahitaji bidhaa/huduma husika ni jambo la kupoteza muda na kujitafutia
matatizo yasiyo ya msingi kama vile msongo wa mawazo na kukata tamaa ya
maisha.
Wajasiriamali waliofanikiwa hujikita zaidi
kutafuta masoko kwa watu wanaohitajika au wanaohitaji bidhaa husika,
hivyo kutumia muda vizuri na rasilimali zilizopo.
Pindi
wajasiriamali wa aina hii wanapogundua kuwa wanakidhi mahitaji ya
wateja wao hutafuta njia au mbinu za kuhakikisha wanawakamata na
kuwakumbatia wasiwaponyoke.
Wajasiriamali hawa hufanya
kila juhudi ya kuanzisha uhusiano mzuri wa muda mrefu kwani tunaambiwa
kuwa mjasiriamali mzuri ni yule anayeona bidhaa yake kupitia mahitaji au
dhima ya mteja wake.
Kufikiria juu ya biashara yako
ikiwa ni pamoja na kufikiria kile kinachoendela nje ya biashara yako
hasa kile kinachohusu au kinachoshabihiana na biashara yako ili kuwa na
uelewa mpana wa mambo mbalimbali yanayohusu shughuli unazozifanya.
Kufanya
uchambuzi wa kina juu ya washindani wako wa biashara siyo tu
kunakusaidia kujua unayeshindana naye bali pia kunakusaidia kujua
matatizo au makosa yanajitokeza katika biashara yako ikiwa ni pamoja na
tafsiri ya kina juu ya biashara yako kwa lengo la kuleta ufanisi katika
utendaji kazi wako.
Ingawa si vizuri kufikiria makosa
au kuanguka kwako kulikotokea siku za nyuma, ni vizuri pia ukatumia
udhaifu au anguko la kipindi cha nyuma kama funzo la kuendesha mambo
yako kwa mafanikio kwani wahenga wanasema binadamu hujifunza kutokana na
makosa. Mjasiriamali wa kweli haogopi kushindwa, bali anafikiria zaidi
namna ya kupata njia mbadala ya kurekebisha makosa yaliyotokana au
yanayotokana na mchakato mzima wa shughuli za kijasiriamali kwa lengo la
kupata mafanikio zaidi.
No comments:
Post a Comment