Kwa
wanaofanya biashara na ambao kwa kiasi wamefikia pazuri wanajua vema kwamba
kuanzisha biashara au kuendesha biashara si jambo rahisi. Watu wengi hugundua ugumu wa kuendesha
biashara baada ya kuanza na si kabla. na pia watu wengi wanachukulia suala la
Ujasiriamali kama jambo jepesi kwa
sababu tu wana uwezo wa kupata
mitaji. Wanafikiri wanaweza kufanya
chochote na kupata mafanikio katika biashara, kumbe kuna mambo mengi ya
kuangalia. zifuatazo ni funguo tano za mafanikio yako katika biashara na
Ujasiriamali.
1. Kuwa na dira.
Dira inakuwezesha kufika kule
unakotaka kwenda. unapaswa kuweka malengo juu ya kule unakotaka kufika baada ya
muda fulani, pia tambua kuwa changamoto unazohisi zitakukumba sambamba na
suluhu sahihi. ukiwa na malengo itakuwa rahisi
sana kukabiliana na vikwazo unapokuwa safarini. Uchunguzi unaonyesha
kwamba Watu wengi huweka malengo huku wakisahau au kupuuzia adha zinazoweza
kuwakumba au zilizowakumba watu wengine waliokuwa na malengo kama yao. Kuwa na
dira na kufikia mafanikio yako.
2. usishindane na waliofanikiwa.
Hili uweze kupata mafanikio katika
biashara na Ujasiriamali hakikisha unawafanya waliofanikiwa wajione wapo juu.
Kama unataka kuwashangaza basi usionyeshe ujuzi wako wote. Kuwapa waliofanikiwa
heshima yao kutakufanya upate msaada na hatimaye ufikie kiwango cha juu cha
mafanikio bila ya kupata taabu nyingi.
3. tenda.
Mafanikio unayopata
kupitia maneno hayafai kitu. usishindane juu ya uwezo wako wa maneno
bali, acha matendo yaongee. Mafanikio
makini ni yale utakayoyapata
kupitia matendo yako, na si kwa wingi wa maneno yako. Uhalisia wa matendo
huonyesha umakini wako kwa jamii inayo kuzunguka. utasifiwa kwa kadiri ya
juhudi zako za hali na mali kwa kutatua changamoto zinazokusonga, si kwa kupiga
domo.
4. Tafuta msaada.
Kufanikiwa kwako kunategemea mchango
utakaoupata kutoka kwa wale wanaokuzunguka
kwa mfano mazingira na marafiki. tumia busara, ujuzi na maarifa ya wale
unaofanya nao kazi ili uweze kusonga mbele. fahamu kuwa Msaada haupunguzi tu
nguvu, bali pia huongeza ufanisi na kuimarisha urafiki. utapata fadhila kutoka
kwa wasaidizi wako, ndipo jamii husika. Hivyo, waachie watu wengine yale
wanayoweza kufanya kwa ufanisi.
5. Malengo.
Ili uweze kufikia mafanikio makubwa katika biashara na Ujasiriamali , unahitaji kuwa na malengo kwani bila malengo ni vigumu kuweza kufanikiwa katika Ujasiriamali. Asante kwa kusoma makala hii, nakutakia kila la kheri katika safari ya kuboresha maisha yako na kuweza kufikia mafanikio makubwa katika biashara na Ujasiriamali. TUPO PAMOJA
No comments:
Post a Comment