Sunday, 26 June 2016

Video: UBORA WA HAZARD WAIPELEKA UBELGIJI ROBO FAINALI EURO 2016

Hazard-Belgium


Star wa Chelsea Eden Hazard alifunga bonge la goli wakati Belgium ikiisambaratisha Hungary na kufuzu kucheza robo fabo fainali ya michuano ya Euro 2016 ambapo itacheza dhidi ya Wales.
Hazard alikuwa vizuri kwenye mchezo huo, alipenya kwa wachezaji wawili akitokea upande wa kushoto wa uwanja na kutengeneza bao lililofungwa na Michy Batshuayi.
Mchezaji wa Tottenham Toby Alderweireld aliifungia Ubelgiji kwa kichwa kabla ya Michu Batshuayi kuongeza bao linguine na kuiweka Ubelgiji mbele kwa bao 2-0.
Hazard alifunga goli la aina yake dakika ya 80 kabla ya Yannick Carrasco kupachika bao la nne dakika za lala salama.
Ubelgiji inataraji kucheza na Wales kwenye mchezo war obo fainali siku ya Ijumaa kwenye mji wa Lille.

No comments:

Post a Comment