Nasema wivu ni ugonjwa kwa nini, wivu unaweza sababisha ugomvi, wivu unaweza leta maumivu kwako au hata kwa mpenzi wako, ndugu jamaa na marafiki wivu unaleta chuki na hata wengine kuchukia mapenzi nakuamua kuwa pekeyao, tayari inaleta matatizo ya kisaikolojia
Nini Ufanye kuzuia wivu uliopitiliza
- Mwamini mwenza wako
Inawezekana ikawa ni kazi ngumu kidogo lakini, hakuna dawa nzuri ya wivu kama kuamini mpenzi wako ni muaminifu na hawezi kukusaliti hata kama unajua ni ngumu kujipa moyo jua ya swala hilo.
- Acha kujifananisha na wengine
- Jiandae Kuishi Maisha Bila Mpenzi Wako
Ndio, najua inaonekana kama ujinga hivi ila sio ukiwa na wivu mara nyingi kitu kinachokuja kichwani ni uoga na unawaza utaishi vipi bila ya mtu Yule, sasa ni vizuri ukawa huru sababu siku akiondoka mtu Yule unaweza changanyikiwa,
Wivu unaondoa mapenzi na unaleta chuki hasira, na mapenzi yanahitaji zaidi uhuru wa nafsi usiwe na uoga wa kumpoteza mtu Yule kwa sababu tu unahisi akiondoka utakufa, jiandae kisaikologia hii itakusaidia kuishi kwa amani kwani hutokuwa na wasiwasi na itapunguza wivu.
- Usimfanyie Mtu Makusudi
- Acha Kuwaza Vitu ambavyo Havipo
Tunaita “Imagination” watu huwaza sana na kupata picha zao wenyewe kichwani ambazo zinaleta hofu au hata kusababisha kuto kumuamini mtu kabisa, sababu tu unawaza vitu sivyo na ukasababisha matatizo lakini badala yake unaweza tumia mawazo yako kuwaza vitu chanya juu ya mapenzi yenu na usiingie katika matatizo
No comments:
Post a Comment