MGOMBEA
wa kiti cha urais wa kupitia chama cha Republican nchini Marekani,
Donald Trump, amesisitiza kuwa, mauaji ya watu 50 yaliyotokea kwenye
Klabu ya wapenzi wa jinsia moja, yamethibitisha msimamo wake wa kutaka
waislamu wapigwe marufuku kuingia humo.
Katika
hotuba yake kwenye jimbo la New Hampshire, Trump amesema mfumo wa Idara
ya uhamiaji nchini Marekani, umeruhusu familia ya Omar Marteen,
aliyetekeleza mauaji hayo kuingia nchini Marekani.
Alidai kuwa, bado mfumo huo umeendelea kuruhusu wauaji wengine kuingia nchini humo bila vikwazo.
Alisema, sababu moja wapo inayochochea muuaji kuwepo nchini Marekani, ni familia ya Marteen kuingia nchini humo.
Aliongeza
kuwa, mfumo wa idara ya uhamiaji isiyotekeleza wajibu wake, bado
hairuhusu kujua ni nani anayepaswa kuingia Marekani ili raia wa nchi
hiyo walindwe.
Kwa
upande wa Mgombea urais kupitia Democratic, Hillary Clinton, akitoa
risala za pole kwa waathiriwa wa mkasa huo, alisema Trump ni kama mtoto
anayesema ovyo kwa namna anavyougeuza mkasa huo wa kitaifa kujipongeza
binafsi.
Akizungumza jimboni Ohio, Hillary, amekosoa mpango wa mpinzani wake ambaye ni Trump, kuwazuia waislamu kuingia Marekani
“Hatua
hiyo ya uchochezi ya vitisho kuzuia familia na marafi ki wa kiislamu
kuingia marekani, pia mamilioni ya wafanyabiashara na watalii waislamu
kuingia nchini, inaumiza sehemu kubwa ya waislamu wanaopenda uhuru na
kuchukia ugaidi,” alisisitiza.
Naye
Rais wa Marekani, Barack Obama alisema, hakuna ushahidi kuwa
aliyetekeleza mashambulizi hayo alikuwa sehemu ya mpango mkubwa wa
mashambulizi.
Obama
alieleza kwamba, shambulio hilo lilisukumwa na msimamo binafsi wa
mshambuliaji huyo na hakuna ushahidi kuwa, Marteen alipata maelekezo
kutoka nje ya nchi kutekeleza mauaji.
Lakini,
Mkurugenzi wa shirika la kijasusi la FBI,James Comey, alisema kuna
ishara kuwa Marteen alishawishika kupitia mitandao ya intaneti ila bado
haijajulikana kama kijana huyo alikuwa anaunga mkono kundi gani la
kigaidi.
Comey
alisema, muuaji huyo alieleza kuunga mkono kundi la wanamgambo wa Dola
ya Kiislamu (IS) pamoja na kundi hasimu na IS la Al Nusra kutoka nchini
Syria.
Katika hatua nyingine,Silaha mbili zilizotumiwa na Marteen zimebainika kununuliwa kwenye kituo cha kuuza silaha.
Mmiliki wa duka hilo Edward Henson, alisema Marteen alipitia taratibu zote zinazopaswa kufuatwa wakati wa kununua silaha hizo.
Naye
mke wa zamani wa Marteen, Sitora Yusufi y, amemwelezea mumewe kama mtu
aliyekuwa na tabia za ugomvi ya kutaka kupiga watu lakini hakuwa na
itikadi kali za kidini.
Tukio
hilo lililohusisha mauaji ya watu 50 na kujeruhi wengine zaidi ya 53
yalitekea kwenye klabu ya starehe ya mashoga iliyopo Frolida Jumapili ya
wiki iliyopita.
Marteen,alivamia kwenye klabu hiyo kisha kuwafyatulia risasi mfululizo watu waliokuwepo ndani.
Wakati akitekeleza mauaji hayo, Marteen aliwateka nyara watu wengine zaidi ya 30 ambao waliokolewa na polisi.
Mtuhumiwa
huyo ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi, ilielezwa alishawahi
kuhojiwa na maofisa usalama mwaka 2013 na 2014 akihusishwa na makundi ya
kigaidi.
No comments:
Post a Comment