Roboti kwa jina
Pepper, iliyotengenezwa kuelewa hisia za watu inatarajiwa kuanza kazi
mpya kama karani wa mapokezi katika hospitali mbili nchini Ubelgiji.
Roboti
hiyo itakuwa ya kwanza kuhudumu katika jumba la matibabu baada ya
roboti nyengine kuwekwa katika maduka ya uuzaji bidhaa, benki na vituo
vya treni.Hospitali moja inamipango ya kuajiri roboti zaidi kwa miaka 10 ijayo.
Baadhi ya wataalamu wamehoji umuhimu wa roboti za kijamii kama vile Pepper.
Roboti hiyo inaurefu wa kina futi nne na inauwezo wa kutambua sauti za binadamu kwa lugha 20 na inauwezo wa kubaini iwapo inazungumza na mwanamume, mwanamke au mtoto.
No comments:
Post a Comment