Mbunge
wa Viti Maalumu (CCM), Fakharia Khamis amehoji bungeni adhabu gani
askari anapewa ikiwa atashindwa kutoa saluti kwa mbunge.
Katika
swali la nyongeza mbunge huyo alitaka kujua maana ya saluti kwa askari
ni nini, na viongozi gani wa uraiani wanaotakiwa kupigiwa saluti katika
mhimili wa Bunge, Serikali na Mahakama.
Akijibu
swali la mbunge huyo, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William
Ole Nasha kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alisema Serikali
imetangaza adhabu ya kuwakata mishahara na adhabu nyingine, askari
polisi wote nchini ambao hawatawapigia saluti wabunge wa Bunge la
Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Ole
Nasha alisema kumpigia saluti mbunge ni jambo la lazima kwa askari kwa
kuwa lipo kwenye moja ya masharti yao, hivyo kutokufanya hivyo ni
kushindwa kutii kiapo cha uaminifu wao.
“Askari
asipotoa saluti unatakiwa kumripoti kwa kiongozi wake ambapo atapewa
adhabu ikiwamo kukatwa mshahara, kupigishwa paredi, kufanya usafi katika
maeneo ya vituo na adhabu nyingine nyingi zinazofanana na hizo,” alisema Ole Nasha.
Alisema
saluti ni salamu ya kijeshi ambayo hutolewa na askari kwa mujibu wa
kanuni za kudumu za utendaji za jeshi la polisi (Police General Orders
–PGO No 102).
Naibu
Waziri alisema sheria hiyo imewataja askari wa vyeo vyote kuwa
wanatakiwa kupiga saluti kwa Rais wa Jamhuri na Rais wa Zanzibar, Makamu
wa Rais na Makamu wawili wote wa Zanzibar, majaji wakuu wa Muungano na
Zanzibar.
Wengine
ni Spika wa Muungano na Zanzibar, mawaziri wote wa Jamhuri na Zanzibar,
makatibu wa Bunge na Baraza la Wawakilishi, wabunge wa muungano na
wawakilishi wanapokuwa kwenye maeneo yao, wakuu wa mikoa, majaji
wanapokuwa kwenye maeneo yao na kwa nafasi zingine ni wakuu wa wilaya na
mahakimu kwenye maeneo yao.
No comments:
Post a Comment