Eritrea
na Ethiopia zimetupiana lawama kwa kuanzisha mapigano mwishoni mwa juma
baina ya majeshi yake katika eneo la mpakani linalotumiwa na nchi zote
mbili la Tsorona.
Eritrea
na Ethiopia zimetupiana lawama kwa kuanzisha mapigano mwishoni mwa juma
baina ya majeshi yake katika eneo la mpakani linalotumiwa na nchi zote
mbili la Tsorona, ikiashiria kuendelea kwa mgogoro wa mpaka uliochochea
vita baina ya mataifa hayo mawili mwaka 1998 hadi 2000.
Ethiopia
imesema kwamba hali ilitulia hapo jana, baada ya wakaazi wanaoishi
upande wa nchi hiyo kutoa taarifa za kusikika kwa milipuko iliyodumu
siku nzima ya Jumapili hadi Jumatatu asubuhi.
Eritrea
nchi iliyo Pembe ya Afrika, ilijipatia uhuru kutoka mikononi mwa
Ethiopia mnamo mwaka 1991. Takribani watu 70,000 waliuawa katika vita ya
kugombea mpaka baina ya mataifa hayo mawili.
Waziri wa
habari wa Eritrea amesema kwamba serikali ya Ethiopia ilianzisha
mashambulizi dhidi ya nchi yake katika eneo la mbele la Tsorona.
Msemaji
wa Umoja wa Mataifa amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa
katibu mkuu Ban Ki-moon anao wasiwasi juu ya mapigano hayo na tayari
anataka kuzifikia pande zote mbili.
Amesema
kwamba "katibu mkuu anazitaka serikali zote kujizuia na kufanyia kazi
utatuzi wa tofauti zao kwa njia ya amani, ikiwemo utekelezaji wa
makubaliano ya amani waliyosaini mwaka 2000" amesema waziri huyo.
Umoja wa
Mataifa ulipeleka kikosi cha kufuatilia makubaliano ya kusitishwa kwa
mapigano mwaka 2000 katika mpaka baina ya nchi hizo mbili , lakini hata
hivyo ilikiondoa kikosi hicho 2008 kutokana na vikwazo vilivyowekwa na
Eritrea na hivyo kushindwa kufanya kazi kwa ujumbe huo.
Ethiopia kwa upande wake nayo imekanusha kuanzisha chokochoko ikisema kwamba ni majeshi ya Eritrea yaliyoanzisha fujo hizo.
Waziri wa
habari wa Eritrea Yemene Ghebremeskel hakuwa na maoni juu ya majeruhi
au taarifa nyingine juu ya mashambulizi hayo.Maafisa wa Ethiopia nao
hawajatoa taarifa ikiwa kulikuwa na majeruhi.
Umoja wa
Mataifa unaishutumu Eritrea kwa ukiukwaji wa muda mrefu wa haki za
huduma za kitaifa ambapo raia wa nchi hiyo hutumia muda mrefu wakilipwa
ujira mdogo kwa mujibu wa sheria.
Charlotte
King, mchambuzi mwandamizi wa Afrika katika kitengo cha intelijensia ya
uchumi anasema wakosoaji wa Eritrea wataona kama nchi hiyo inajaribu
kukwepa tahadhari ya jumuiya za kimataifa dhidi ya uhalifu wa ubinaadamu
na kuhalalisha mahitaji yake ya kijeshi.
Eritrea
iliyo na vikwazo vya Umoja wa mataifa inasema mataigfa yenye nguvu
yameshindwa kuishinkiza Ethiopia kukubaliana na usuluhishi wa kimataifa
unaotawala mpaka huo. Ethiopia imesema inataka mazungumzo kwa ajili ya
utekelezaji.DW
No comments:
Post a Comment