Golikipa mkongwe wa TP Mazembe Robert Kidiaba hakuacha kusema wanam-miss Mbwana Samatta kutokana na uwezo wake wa kupachika mpira wavuni, na kuisadia Mazembe kuibuka na ushindi.
Kidiaba anasema kuondoka kwa Samatta kuwewafanya wapoteze mchezezaji muhimu kutokana na uwezo wake.
“Tumepoteza mchezaji muhimu sana anayeweza kufunga magoli dhidi ya timu yoyote, Samatta anaweza kufunga magoli lakini ameshaenda”, alisema Kidiaba ambaye alibwagwa na Samatta kwenye kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani mapema mwaka huu.
Kidiaba akatoa neno kuhusu Thomas Ulimwengu ambaye sasa anachezeshwa kama mshambuliaji wa kati kwenye kikosi cha Mazembe.
“Sasahivi matumaini yetu yapo kwa Thomas (Ulimwengu) yeye ndiyo anamrithi Samatta”.
Anaizngumziaje Yanga SC?
“Yanga ni timu kubwa hapa Tanzania, sisi tuliwaheshimu kabla ya na tukasema timu zote ambazo zimefuzu hatua hii ni kubwa ndiyo maana tumewafunga goli moja.”
“Lakini Yanga ni timu nzuri mimi nimewaona leo lakini nimeona wachezaji wanacheza vizur.i”
Golikipa anayemuweka benchi je?
“Kipa mzuri, bado mtoto mimi sasa nimezeeka yeye bado anamuda wa kucheza na mimi nitamsimamia aendelee na mazoezi na kazi yake.”
No comments:
Post a Comment