
EURO 2016
Ratiba/Matokeo:
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Jumatatu Juni 27
Italy 2 Spain 0
England v Iceland (2200, Stade de Nice)

NDANI ya Stade de France Mjini Paris Nchini France, Mabingwa Watetezi Spain Leo wamevuliwa Taji lao baada ya kuchapwa 2-0 na Italy katika Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16.

Italy walifunga Bao lao la Kwanza Dakika ya 33 baada ya Eder kupiga Frikiki ambayo iliokolewa na Kipa De Gea na kumkuta Giaccherini alieucheza Mpira na De Gea kuupiga tena kwa Mguu wakati akiwa amelala chini lakini ukamkuta Giorgio Chiellini alieutumbukiza wavuni.

Bao hilo lilidumu hadi Haftaimu.
Kipindi cha Pili Spain walikuja juu lakini walishindwa kuipenya ngome ngumu ya Italy ikongozwa na Chiellini na Bonucci.

Lakini Italy nao walikuwa hatari mno kwa kaunta-ataki ambazo mara kadhaa Spain waliokolewa na umahiri wa Kipa wao David De Gea.
Hata hivyo, katika Dakika ya 92, pasi ndefu ya Insigne toka Winga ya Kushoto kwenda Winga ya Kulia ilimkuta Darmian ambae Krosi yake ilimbabatiza Sergio Ramos na kumfikia Graziano Pelle ambae alikuwa uso kwa uso na Kipa De Gea na hakufanya kosa kukwamisha Mpira wavuni na kuipa Italy Bao lao la Pili.

Sasa Italy wametinga Robo Fainali ambapo watacheza na Germany hapo Jumamosi.
Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya EURO 2016 itamalizika Leo Usiku huko Mjini Nice kwa Mechi kati ya England na Iceland.

VIKOSI:
Italy (Mfumo 3-1-4-2) Buffon; Barzagli, Bonucci, Chiellini; De Rossi; Florenzi, Parolo, Giaccherini, Di Sciglio; Pelle, Eder.
Akiba: Sirigu, Marchetti, Darmian, Ogbonna, Candreva, Zaza, Motta, Immobile, Sturaro, Insigne, Bernardeschi, El Shaarawy.
Spain (Mfumo 4-1-2-3) De Gea; Juanfran, Pique, Ramos, Jordi Alba; Busquets; Fabregas, Iniesta; Silva, Morata, Nolito.
Akiba: Casillas, Rico, Azpilicueta, Bartra, Koke, Lucas Vazquez, Pedro, Bellerin, Thiago, San Jose, Bruno, Aduriz.

REFA: Cuneyt Cakir (Turkey)
EURO 2016
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Jumamosi Juni 25
Switzerland 1 Poland 1 (Baada Dakika 120 1-1, Poland yasonga Penati 5-4)
Wales 1 Northern Ireland 0
Croatia 0 Portugal 0 [Baada Dakika 120, Portugal yashinda 1-0]
Jumapili Juni 26
France 2 Republic of Ireland 1
Germany 3 Slovakia 0
Hungary 0 Belgium 4
Jumatatu Juni 27
Italy 2 Spain 0
England v Iceland (2200, Stade de Nice)

ROBO FAINALI
Alhamisi Juni 30
Robo Fainali ya 1, (2200, Stade Velodrome, Marseille)
Poland v Portugal
Ijumaa Julai 1
Robo Fainali ya 2, (2200, Stade Pierre Mauroy, Lille)
Wales v Belgium
Jumamosi Julai 2
Robo Fainali ya 3, (2200, Stade de Bordeaux)
Germany v Italy
Jumapili Julai 3
Robo Fainali ya 4, (2200, Stade de France, Paris)
France v England v Iceland
NUSU FAINALI
Jumatano Julai 6
Mshindi Robo Fainali ya 1 v Mshindi Robo Fainali ya 2 (2200, Stade de Lyon)
Poland au Portugal v Wales au Belgium
Alhamisi Julai 7
Mshindi Robo Fainali ya 3 v Mshindi Robo Fainali ya 4 (2200, Stade Velodrome, Marseille)
Germany/Italy v France/England au Iceland
FAINALI
Jumapili Julai 10
(2200, Stade de France, Paris)
No comments:
Post a Comment