Kadri Teknolojia inavyozidi kukua kila
siku katika upande wa usafirishaji ndivyo ufumbuzi wa baadhi ya
changamoto zinavyozidi kupatiwa majibu, kama ilivyo kwa Tanzania
ilivyoleta mabasi yaendayo haraka ili kuepuka foleni, ndivyo hivyo
imetokea Beijing China ambapo wao wameweza kutengeneza basi la umeme
lenye uwezo wa kupita juu ya magari mengine.
Kutokana na China kuwa nchi yenye watu
wengi zaidi Duniani, hivyo basi hilo linalotajwa kubeba watu 1200 kwa
mara moja, linatajwa kuwa ufumbuzi sahihi wa msongamano wa magari
barabarani, basi hilo lilifanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza May 19
2016.
No comments:
Post a Comment