Mkongwe wa Bolton Wanderers na timu ya taifa ya Nigeria Jay-Jay Okocha amefunga moja ya magoli mazuri wakati ma-legend wa Bolton walipocheza mcheza mechi ya hisani kwa ajili ya kuchangisha pesa kwa ajili ya timu na jamii.
Okocha alionesha uwezo mkubwa kwenye game hiyo na kuwakumbusha mashabiki enzi za ujana wake. Alifunga magoli mawili (goli moja kwa kila timu) na kufanya mambo mengi uwanjani ambayo mashabiki walizoea kuona wakati akiwa bado kwenye ubora wake.
Goli la kwanza la Okocha liliwakumbusha watazamaji enzi za ujana wa Okocha kutokana na ubora wa goli lenyewe ambapo kiungo huyo wa zamani wa The Eaggles aliujaza mpira kambani akiwa umbali wa takribani mita 20 kutoka lilipo goli.
Shuhudia goli alilofunga Okocha wakati wa mechi ya wakongwe wa Bolton Wanderers
No comments:
Post a Comment