Thursday, 19 May 2016

Unajua ni jinsi gani watu hukabiliana maumivu ya mapenzi kutokana na n yota zao.

Watu wachache huamini katika nyota, hata mimi huwa siamini ila kitu kimoja kime nifurahisha na  nikaona si mbaya kushare na watu. Kuna mapenzi na kuna kuumizwa  na kila binadamu anajinsi yake anavyojua kukabiliana na maumivu hayo.  Je unajua ni kwa jinsi gani watu hukabili maumivu ya mapenzi  kutokana na nyota zao.
Kondoo/Punda. (Aries)
Ni watu washeshi na wanapendwa na wengi, ila wanahasira  za  karibu sana, ukimuumiza mtu wa Nyota hii utajuta sababu hato ogopa kumwambia mama yako, boss wako au rafiki zako kwa kiasi gani umekuwa mpumbafu kwake.
Ng’ombe (Taurus)
Hawa wanaitwa Silent Killer hawaonyeshi maumivu na wanaweza kukaa kimya ila wanapanga kisasi ndani kwa ndani, wanaweka vitu moyoni  bila kukuonyesha wanaumia. Watu wasiosema sio wazuri kuwa nao karibu.
Mapacha (Gemini.)
Ukiwa na mpenzi wa nyota hii yeye ni mtu wa kuvunja vunja akiwa na hasira, kwahiyo weka vitu vyako mbali na macho yake. Kwani akigundua umemuumiza,umemsaliti  atavunja Tv, Atachana nguo zako atakuchomea gari  na mengine mengi.
Kaa (Cancer)
Hawa ni watulivu sana ila siku ukimtibua kwa usaliti wa mapenzi hatoshindwa kumwambia kila mtu aliekuwa anasema wewe ni mtu mzuri , ni watu wa hasira pia kama mtu akivuka mipaka.
Simba (Leo)
Hawa hutumia udhaifu wako na maumivu yako hasa akijua umemsaliti atakutesa kisaikologia kwani hatokuwa mbali na wewe ila hatahakikisha kila wakati unajisikia vibaya juu ya ulichofanya, hutokuwa na amani hata wakisamehe hawasahau
Mashuke (Virgo)
uchunguza nini kimekufanya uwasaliti, wao watakufatilia kila unachofanya nani unaongea nae nani yuko karibu na wewe mpaka wajue kilichokupa jeuri.  Na ni watu wakisha amua kuendelea mbele hawarudi nyuma

No comments:

Post a Comment