Sunday, 22 May 2016

TOP 10 YA WACHEZA SOKA MAARUFU ZAIDI DUNIANI

Ronaldo-ballon
10. Iker Casillas – Porto
Kipa huyu wa zamani wa Real Madrid, ambaye kwa sasa anacheza Porto ya Ureno, ameshinda takriban kila kitu katika maisha yake ya soka kwenye ngazi ya timu ya taifa ya (Hispania) na klabu pia.
Tangu aondoke Real Madrid na kuhamia Porto, Iker Casillas amegeuka kuwa kipa mbovu katika historia ya klabu hiyo kwa miaka takriban 15, akifungwa magoli 30 katik michezo 34 ya ligi, licha ya ubovu wake kwa sasa, Casillas amebaki kuwa moja ya wachezaji wenye umaarufu mkubwa ulimwenguni.
  1. Gareth Bale – Real Madrid
Mchezaji huyu wa zamani wa Tottenham bado anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliyenunuliwa kwa gharama kubwa zaidi duniani kutoka Spurs kwenda Real Madrid. Katika msimu wake wa kwanza, Bale aliingoza Madrid kuchukua ubingwa wa UEFA kwa mara ya kumi baada ya kuutafuta kwa miaka mingi, huku vile vile akiiongoza timu yake ya taifa ya Wales kwenda michuano ya EURO mwaka huu.
  1. Andres Iniesta – Barcelona
Iniesta ni moja ya kati ya wachezaji wenye nahati kubwa katika historia ya mpira duniani, ameshinda kila kitu akiwa na Barcelona na na Hispania, kizazi chake kimebeba ndoo ya La Liga kati ya 24 ambazo Barcelona wametwaa.
  1. James Rodriguez – Real Madrid
Si watu wengi walimjua Mcolombia huyu kabla ya kuwa mfungaji bora wa kombe la dunia mwaka 2014 huko nchini Brazil na na kuibuka kidedea kwa kunyakua tuzo ya goli bora la michuano ya hiyo dhidi ya Uruguay. Uhamisho wake kutoka Monaco kwenda Real Madrid ulizidi kumuongezea umaarufu.
  1. Mesut Ozil – Arsenal
Kiungo huyu wa Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani sio tu mchezaji mbunifu zaidi katika Ligi Kuu ya England lakini pia ni maarufu ulimwenguni kote. Katika msimu huu EPL, Ozil ametengeneza nafasi nyingi kuliko mchezaji yeyote na kuipeleka Arsenal nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi juu ya mahasimu wao wakubwa Tottenham Hotspurs.
  1. Luis Suarez – Barcelona
Mshambuliaji huyu wa Barcelona ama hakika ameonesha kwamba kwa sasa ndiye mshambuliaji wa kati bora zaidi ulimwenguni baada ya kufunga magoli 53 katika mchezo 47 kunako klabu hiyo simu huu, akiwazidi Lionel Messi na Neymar. Magoli 40 ya ligi msimu huu kwa staa huyo wa Uruguay yamethibitisha kwamba si tu ameibuka kidedea La Liga bali vile vile Ulaya kwa ujumla. Umaarufu wake kwenye mitandao ya kijamii umeongezeka kwa 20% katika wiki chache zilizopita baada ya kuonesha kiwango bora msimu huu.
  1. Zlatan Ibrahimovic – Paris Saint Germain
Huyu ni mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden. Anasifika kwa ubora wa hali ya juu awapo uwanjani kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusumbua mabeki, amejaaliwa mwili uliojengeka kimchezo, kimo stahiki kwa mshambuliaji na uwezo mkubwa wa kufumani nyavu.
Ibrahimovic ameshinda mara nne mfululizo kombe la Ligi Kuu Ufaransa maarufu kama Ligue 1, amekuwa mfungaji bora wa ligi hiyo kwa misimu mitatu mfululizo tangu ajiunge na Paris Saint Germain mwaka 2012. Amejiwekea historia kubwa klabuni hapo na kwa sasa anahesabika kama legend kwa sasa baada ya kutanabaisha kuondoka msimu huu.
Anasifika kwa nukuu (quotes) zake za kusisimua na amekuwa moja ya washambuliaji waliocheza kwenye vilabu vingi vikubwa duniani ikiwemo Barcelona.
  1. Lionel Messi – Barcelona
Wachezaji wengi,mashabiki na wachambuzi wa soka wanamtazama Lionel Messi kama mchezaji bora bota ulimwenguni na kusadiki kama ndiye mchezaji bora wa muda wote duniani.
Nyota huyo wa Argentina ni mchezaji pekee katika historia ya soka duniani kuwahi kutokea baada ya kushinda tuzo ya mchezajo bora wa dunia (Ballon d’Or) mara tano, huku miaka minne akishinda mfululizo.
Mpaka sasa katika maisha yake ya soka, Messi amecheza kweny klabu ya Barcelona pekee na kuipa mafanikio makubwa kwa kipndi cha muongo mmoja.
 
  1. Neymar – Barcelona
Mbrazil huyu mwenye kipaji cha aina yake, ana uwezo mkubwa sana hasa kuwanyanyasa mabeki wa timu pinzani bila ya kusahau uwezo wake mkubwa wa kufunga. ameshika nafasi ya tatu nyuma ya Messi na Ronaldo katika tuzo ya Ballon d’Or January mwaka huu.
  1. Cristiano Ronaldo – Real Madrid
Cristiano Ronaldo ni mfungaji wa muda wote wa klabu ya Real Madrid, anasifika kwa utanashati wake ndani na nje ya uwanja. Mchezaji huyu wa zamani wa Manchester United bila shaka ni moja ya wachezaji hodari linapofika suala upachikaji mabao. Amevunja rekodi nyingine msimu huu baada ya kufunga zaidi ya mabao 50 kwa misimu sita mfululizo.
Ndiye mchezaji mwenye mashabiki wengi zaid kwenye mitandao ya kijamii akiwa na zaidi ya mashabiki milioni 211.7 Facebook, Twitter na Instagram. Ameidizi mpaka klabu yake.

No comments:

Post a Comment