Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa mashauriano wa Bodi
ya Usajili wa Makandarasi Nchini (CRB) leo tarehe 26 Mei, 2016 katika
ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Mkutano
huo wa mwaka wa mashauriano na wadau wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi
unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya Makandarasi na wadau wa Sekta ya
Ujenzi wapatao 1000 na utafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 26 Mei,
2016 hadi tarehe 27 Mei 20l6.
Kaulimbiu
ya mwaka huu ni ‘Juhudi za Makusudi za Kukuza Uwezo wa Makandarasi
Wazalendo kwa Maendeleo Endelevu ya Kiuchumi; Changamoto na Mustakabali
Wake’.
Lengo
la mkutano huu ni kuwakutanisha wadau wa Bodi ya Usajili Makandarasi na
Sekta ya Ujenzi ili kujadili changamoto zinazowakabili na kuweka
mikakati ya kuwajengea uwezo Makandarasi Wazalendo.
Imetolewa;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment