Mwanamme mmoja amekamatwa ndani ya makao ya kifalme nchini Uingereza ya Buckingham baada ya kuvuka ua.
Mwanamme
huyo wa umri wa miaka 41 alipatikana katika uwanja wa kasri hilo dakika
saba baada ya ving'ora kuanza kulia siku ya Jumatano jioni.Mshukiwa huyo ambaye hakuwa na silaha yoyote alikamatwa kwa kushukiwa kuingia eneo linalolindwa na sasa yuko kizuizini.
Kumeshuhudiwa utata mara kadha kwenye ulinzi wa kasri la Buckingham miaka ya nyuma, kikiwemo kisa cha Michael Fagan ambaye aliingia hadi chumba cha kulala cha Malkia mwaka 1982, na kukaa kwa muda wa dakika 10 akizungumza na malkia kabla ya Malkia kufanikiwa kupiga king'ora wakati mtu huyo alipoomba sigara.
No comments:
Post a Comment