Monday, 28 March 2016

Zimbabwe yairarua Swaziland 4 - 0

y
Mechi za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya afrika zimepigwa jana kwa michezo kadhaa, Zimbabwe imeirarua Swaziland mabao 4-0 huku Afrika ya kati ikiichapa Madascar goli 2-1.
Katika matokeo mengine Equatorial Guinea imechabangwa na mali bao 1-0, na Libya imeizamisha Sao Tome kwa kichapo cha bao 4-0.
Michuano hii inaendelea tena leo kwa michezo mbalimbali, miongoni mwa mechi zitakazo pigwa,Malawi itacheza na Guinea, Ethiopia na Algeria, Rwanda itaikabili Maurtius.
Katika mechi nyingine Togo itakabana koo na Tunisia wakati Angola watakuwa wenyeji wa D.R Congo, Uganda watawakaribisha Burkina faso, Misri watakuwa wenyeji wa Nigeria, Sudan itachuana na Ivory Coast na Niger itamenyana na Senegal,hizo ni miongon mwa mechi zitakazo pigwa hii leo.

No comments:

Post a Comment