Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Profesa Jumanne Maghembe amewasimamisha kazi watumishi watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kuwahamisha wengine 15 kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha na ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa Umma.
Mh.waziri Maghembe amechukua hatua hiyo baada ya kutembelea na
kukutana na wafanyakazi wa mamlaka hiyo na amesema hatua zingine
zitafuata kwa watumishi hao ambao wote watano ni wa idara ya uhasibu.
Kuhusu watumishi wanaohamishwa ambao ni wa idara mbalimbali
ikiwemo uhandisi,utalii na ikolojia Mh.Prof.Maghembe amesema hatua hiyo
inalenga kutoa nafasi ya kuendelea kufanyika kwa uchunguzi zaidi juu ya
tuhuma mbali mbali zinazowakabili.
Mhifadhi wa Mamlaka ya Ngorongoro Bw.Fredy Manongi pamoja na kukiri
kuwa mamlaka inakabiliwa na changamoto mbalimbali amesema kwa sasa
tatizo kubwa ni ujangili unaofanyika katika maeneo ya mipakani japo
amesema wanaendelea kuzikabili.
Hii ni ziara ya kwanza ya Waziri wa Maliasili na Utalii Jumanne
Maghembe katika mamlaka hiyo ambayo amesema ni mwendelezo wa utekelezaji
wa azma ya serikali ya kuimarisha uwajibikaji,ukusanyaji wa mapato na
kuimarisha shughuli za uhifadhi.
No comments:
Post a Comment