Monday, 7 March 2016

Ubishi wa Leo Messi Vs Ronaldo wasababisha Wanaijeria Kuuana India


Story ya kusikitisha inayohusisha kifo cha mtu mmoja kilichotokana na ushabiki wa mpira, kimeripotiwa na gazeti la Hindustan Times.
  Kijana Obinna Micheal Durumchukwa aliyekuwa na umri wa miaka 34 ameripotiwa kuuwawa baada ya ubishani Leo Messi vs Cristiano Ronaldo kuzidi kipimo na kugeuka kuwa ugomvi.
Tukio hilo limetokea huko Nala Sopara, Mumbai nchini India.
  Kwa mujibu wa ripoti, kifo cha Durumchukuwa kilitokea kwenye party ya Birthday yake.
Polisi nchini India wamesema, Durumchukwa alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na rafiki yake Nwabu Chukwuma, 22, katika apartment moja ya kukodi, mahala ambapo walianza kubishana juu ya nani kati ya Messi na Ronaldo ni bora kumzidi mwenzie.
  Durumchukwa akamrushia glass Chukwuma, ambayo ilimkosa na kuvunjika kwenye ukuta. Baada ya hapo Chukwuma akaogopa kipande cha glass na kumkata rafiki yake kwenye koo kwa hasira, ameeleza inspekta wa polisi, Kiran Kabadi wa kituo cha Tulinj.


No comments:

Post a Comment