Msanii wa filamu nchini Tanzania Single Mtambalike maarufu kama Richie ambaye pia alikuwa mshindi wa tuzo za Africa Magic Viewers Choice za nchini Nigeria kwenye kipengele cha Best Indigeous Language Movie/TV Series Swahili kupitia Movie ya Kitendawili amesema kuwa amejifunza mambo kadhaa kuhusu soko la filamu la Nigeria.
Richie ameweka wazi kuwa nigeria wamejipanga na wanapenda vya kwao na kuwataka watanzaniawaige mfano huo ili kuweka soko la nyumbani kwenye ushindani.
“Nimejifunza mengi,wao wako well organized..wana umoja wako wwengi wanapenda vya kwao,na sisi pia tuige hilo”
alisema Richie ambaye pia anadai kuwa wanigeria hawatishi kama watu wanavyodhani na kusema kuwa uwezekano wa kuwashinda upo ikiwa watanzania wakijipanga.
Source:Clouds
No comments:
Post a Comment