Rais
Magufuli ametoa wito huo leo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front Jijini Dar es salaam, ambako
amesali ibada ya Pasaka pamoja na waumini wa kanisa hilo.
Amesema
Mwenyezi Mungu alimtoa mwanae wa pekee Yesu Kristo kuja kuikomboa dunia
bila kuwabagua wanadamu, vivyo hivyo nasi binadamu tunapaswa
kutobaguana, iwe kwa dini zetu, makabila yetu, mitazamo ya kisiasa na
hata rangi zetu.
Aidha,
Rais Magufuli amewakumbusha watanzania kufanya kazi kama ambavyo vitabu
vitakatifu vinasisitiza umuhimu wa kufanya kazi, na amebainisha kuwa
Tanzania yenye neema inawezekana endapo kila mtu atazingatia kufanya
kazi.
“Tukifanya
kazi hatuhitaji hata misaada kutoka nje, nchi hii ina neema nyingi. Kwa
kweli tukifanya kazi kwa bidi nchi yetu inapaswa kuwa inatoa misaada
kwa nchi nyingine na sio kuomba misaada kutoka nchi nyingine” Amesisitiza Dkt. Magufuli.
Rais
Magufuli ambaye amesali kwenye kanisa hilo kwa mara ya kwanza tangu
achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini ikiwa ni
mara yake ya nne kusali katika kanisa hilo hata kabla ya kuwa Rais,
amewaomba watanzania kuendelea kuliombea Taifa lao na pia kumuombea yeye
ili afanikiwe kutekeleza jukumu kubwa na zito la kuiongoza nchi.
Pamoja
na kuongoza maombi ya kumuombea Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth
Magufuli waliohudhuria ibada hiyo, Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya
Mashariki na Pwani, Dkt. Alex Malasusa amempongeza Rais Magufuli kwa
tabia yake ya kupenda kuhudhuria ibada na kuwasihi viongozi wengine
kupenda ibada.
Askofu
Malasusa ameuelezea ufufuo wa Yesu Kristo kuwa jambo la kuleta
matumaini, na hivyo amepongeza mwelekeo wa nchi kwa sasa, huku akisema
Kanisa linaona matumaini kwa Taifa.
No comments:
Post a Comment