Sunday, 6 March 2016

Mwanafunzi Abakwa na Kuuawa kwa Kunyongwa


Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnero iliyopo Tarafa ya Ruponda mkoani Lindi, ameuawa kwa kunyongwa baada ya kubakwa na wanaume wasiofahamika kisha mwili wake kutelekezwa kichakani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga alisema jana kuwa mwanafunzi huyo alikuwa na tabia ya kuruka ukuta usiku na kwenda nje ya shule kufuata wanaume.

Kamanda Mzinga alisema mwanafunzi huyo alipofika kwenye kichaka hicho kilichopo karibu na eneo la Kanisa Katoliki alibakwa na wanaume hao kisha kumuua kwa kumnyonga.

Alisema wanamshikilia mwendesha bodaboda, mkazi wa Kijiji cha Mnero ngongo kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment