Dunia ya soka imepata msiba mwingine siku kadhaa baada ya kifo cha
Johan Cruyff, wana afrika mashariki tuna Msiba mwingine. – golikipa wa
zamani wa Simba, Abel Dhaira hatunae tena.
Golikipa huyo aliyekuwa na miaka 28 aligundulika kuwa na kansa ya tumbo mwanzoni mwa mwaka huu.
Kifo chake kimekuja wakati ambao mkataba wake wa bima ya afya katika
klabu ya IBV Vestmanaeyjar ya Iceland – ulikuwa unamalizika.
Dhaira alianza maisha yake ya soka katika klabu ya Walukuba ya jijini Jinja.
Baada ya hapo alihamia Express, kisha akaenda URA kabla ya kuja kujiunga na Simba Sports Club ya Tanzania.
Aliitumikia klabu ya IBV Vestmanaeyjar football club inayoshiriki ligi ya Iceland premier league mpaka kifo chake.
No comments:
Post a Comment