Monday, 28 March 2016

Dk Shein amteua Balozi Seif Ali Idd Kuwa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar


Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein amemteua Balozi Seif Ali Idd kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa visiwa hivyo.

Kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 39 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Dk Shein amemteua Balozi Idd ambaye alikuwa na wadhifa huo hata kipindi kilichopita.

Uteuzi wa Balozi Idd aliyezaliwa Februari 23, mwaka 1942, ulianza jana ikiwa ni siku nne tangu kuapishwa kwa Shein kuwa Rais wa Zanzibar.

Balozi Idd anakuwa mtu wa pili kuteuliwa na Dk Shein baada ya kuteuliwa kwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said mwishoni mwa wiki.

Dk Shein sasa atakuwa na wakati mgumu wa ama kumteua au kutomteua Makamu wa Kwanza wa Rais ili kukidhi matakwa ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwani hakuna chama cha upinzani kilichokidhi vigezo vya kushirikishwa katika kuunda Serikali

No comments:

Post a Comment