Thursday, 25 February 2016

Serikali haina msalie mtume na wakwepa kodi’


WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philipo Mpango amewataka wafanyabiashara mkoani Arusha, kuhakikisha wanalipa kodi halali ya serikali ya biashara wanazofanya, kwani Serikali ya Awamu ya Tano haina msalie mtume kwa mfanyabiashara atakayekwepa kodi, kwani rungu la sheria litamshukia. Aidha, amesema Serikali haiko madarakani ili kumnyanyasa mfanyabiashara anayelipa kodi halali na wala haiko tayari, kuona watendaji wa Mamlaka ya Mapato (TRA) wanawanyanyasa wafanyabiashara kwa kisingizio cha kodi.
Dk Mpango alisema hayo jana mjini hapa wakati alipokutana na wafanyabiashara wakubwa wa Arusha kwa lengo la kuwaeleza nia ya Serikali ya Awamu ya Tano juu ya ukusanyaji kodi na kujua kero, zinazowasumbua katika ukusanyaji kodi hiyo.

No comments:

Post a Comment