Watoto wawili wa Afrika kusini wanamshitaki muhubiri wa kanisa kubwa na maarufu nchinini Nigeria TB Joshua kwa kifo cha baba yao, wakili wao Bolajii Ayorinde ameiambia BBC.
Baba yao alikua miongoni mwa watu 116 waliokufa wakati jengo la makazi yanayomilikiwa na kanisa hilo lilipoporomoka mjini Lagos mwaka 2014.
Mwaka jana mahakama ya uchunguzi wa vifo iliamuru TB Joshua anapaswa kushtakiwa juu ya kuporomoka kwa jengo, akisema kanisa hilo linahusika kwasababu ya uzembe wa kiuhalifu. Muhubiri TB Joshua na kanisa lake wamekua wakikana kufanya kosa lolote.BBC
No comments:
Post a Comment