Wednesday, 24 February 2016

Cristiano Ronaldo Abadili Mfumo wa Mazoezi na Chakula Ili Adumu Zaidi Kwenye Soka



Cristiano Ronaldo amejitambua kwamba umeanza kuelekea mwishoni mwa maisha yake ndani ya soka – mapema mwezi huu Ronaldo alitimiza miaka 31.
  Pamoja na kwamba bado yupo vizuri kimwili, mwili wake umeanza kutoa ishara za kawaida za maonyo kwa wachezaji ambao wamevuka miaka 30.
Nahodha huyo wa Ureno ameanza kuelewa kwamba anatakiwa kuupa uangalifu mkubwa mwili ikiwa angependa maisha yake kwenye soka yawe marefu na hilo limemfanya Ronaldo aamue kubadili mfumo wa vyakula vyake na kuweka mabadiliko matayarisho yake ya kimwili.
Gazeti la ‘ABC’ limeripoti kwamba staa huyo wa Madrid ameanza kupunguza uzito tangu alipofikisha umri wa miaka 30. Alipofikisha umri huo alishauriwa kitabibu awe anapunguza kilo moja kila mwaka. Tangu January 2015,  ameshapoteza kilo 2 kutokana na mabadiliko aliyofanya kwenye chakula akiwa na lengo la kuiweka spidi ya mwili wake – jambo ambalo hutokea kwa wachezaji ambao hufikisha miaka 30 na kuendelea.
 CR7 kwa sasa ana kilo 78. Na pia amepunguza mazoezi ya ubebaji wa vitu vizito kwa kiasi kidogo kulingana na maelekezo ya ‘trainer’.
Takwimu zinathibitisha kwamba ni kweli ameanza kushuka, ingawa bado anabaki kuwa mchezaji muhimu wa Madrid na Ureno.

No comments:

Post a Comment