WIZARA
ya Fedha na Mipango imetoa sh.bilioni 12.3 kwa ajili shughuli za
mahakama ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Rais Dk. John Pombe Magufuli
aliyoiahidi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mahakama.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Fedha na
Mipango, Dk. Philip Mpango amesema fedha hiyo imetolewa kwa kutimiza
ahadi ya Rais ya uendeshaji wa shughuli za mahakama.
Mpango
amesema kuwa ahadi ya Rais ilikuwa ni ya siku tano ambazo zimetimia kwa
kutoa hundi ya sh.bilioni 12.3 ambazo zitakwenda kufanya kazi
iliyokusudiwa.
Amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango kutokana na ahadi hiyo imefanya kuweka wazi juu ya fedha hizo kwa waandishi wa habari.
Nae
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju amesema
lengo ni kuongeza kasi kwa mashauri yaliyopo kuondoshwa pamoja na
waliokwepa kodi yashughulilikiwe.
Ahadi
ya Rais ilitolewa baada ya maombi ya Jaji Mkuu, Othman Chande katika
maadhimisho ya kuanza kwa mwaka wa mahakama kudai kuwa wana uhaba fedha
za maendeleo katika kuweza kuendesha shughuli za kimahakama.
Waziri
wa Fedha Mipango, Philip Mpango (Katikati) akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na kutimiza ahadi aliyoiahidi
Rais Dkt. John Pombe Josef Magufuli alipoahidi katika maadhimisho ya
siku ya mahakama hapa nchini. Kulia ni Naibu waziri wa katiba na sheria,
Amon Mpanju na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango
Dkt. Servacius Likwelile.
Mtendaji
mkuu wa Mahakama Hussein Kattanga (kushoto)akimshukuru Rais Dkt. John
Pombe Josef Magufuli kwa kutimiza ahadi yake aliyoiahidi siku ya
maadhimisho ya siku ya mahakama. kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
na Mipango Dkt. Servacius Likwelile



No comments:
Post a Comment