Saturday, 9 January 2016

ZIDANE AMEANZA NA 5-0, BALE APIGA 3, BENZEMA ( VIDEO )

Image result for ZINEDINE ZIDANE

 ZINEDINE ZIDANE ameanza vyema himaya yake na Real Madrid walipowatandika Deportivo La Coruna 5-0 katika Mechi ya La Liga Uwanjani Santiago Bernabeu.
Gareth alipiga Bao 3 na Karim Benzema Bao 2 kwenye Mechi ambayo Real hawakucheza vyema sana lakini walionyesha nini Zidane anataka Soka lipi ambalo mwenyewe ametangaza ni la kushambulia tu.
Ushindi huu bado umewaweka Real Nafasi ya 3 kwenye La Liga wakiwa Pointi 1 nyuma ya Atletico Madrid na Pointi 2 nyuma ya Vinara Barcelona huku wao wakiwa wamecheza Mechi 1 zaidi.
VIKOSI:
Real Madrid: Navas; Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo; Modric, Kroos, Isco; Bale, Benzema, Cristiano Ronaldo
Akiba: Casilla, Varane, James Rodriguez, Casemiro, Lucas Vasquez, Jese, Danilo
Deportivo la Coruna
Poroto Lux; Juanfran, Arribas, Sidnei, Navarro; Mosquera, Bergantinos; Faycal Fajr, Carabia, Luis Alberto; Lucas
Akiba: Manu Fernandez, Riera, Dominguez, Laure, Luisinho, Lopo, Jonas.
REFA: Pedro Perez

Jumamosi Januari 9
FC Barcelona 4 Granada CF 0
Sevilla FC 2 Athletic de Bilbao 0
Getafe CF 1 Real Betis 0
Real Madrid CF 5 Deportivo La Coruna 0
Jumapili Januari 10
0005 Levante v Rayo Vallecano
1400 Villarreal CF v Sporting Gijon
1800 Real Sociedad v Valencia C.F
2015 SD Eibar v RCD Espanyol
2015 Las Palmas v Malaga CF
2230 Celta de Vigo v Atletico de Madrid


No comments:

Post a Comment