Mahusiano yako ya nyuma
Ni vigumu sana wapenzi kuelezana historia zao za mapenzi hasa inapokuja swala la umetembea na wangapi? Hapa kama uliambiwa umedanganywa tafiti zinaonyesha wanaume ndo wanajua kudanganya kwenye swala hili kuliko wanawake japokuwa kwa asilimia kubwa wapenzi huwa hawaambiani ukweli kuhusu watu wangapi wameshakuwa na mahusiano nao ya kimapenzi. Kwahiyo ni bora usiulize usijisumbue.
Kipato
Hapa inakuwa shida kidogo kwani hela haina mapenzi, haina undugu na ni mara chache ukute wapenzi wanajua mishahara au kipato cha mwenza wake, wapenzi wengi huwa wanafichana na wengine hata wanadanganya kuhusu madeni waliyonayo ni kawaida sana kwa mapenzi ya sasa hasa hali ya kipato ilivyo ngumu.
Kufurahia Tendo
Wapenzi wengi hawaambiani kweli hasa wanapo kutana kimwili, kama walifurahia au walichukia, wanawake wanasifika kwa kudanganya wameridhika, ila pia wanaume huwa hawasemi kama msichana hayuko vizuri kwenye game, na ndo maana watu baada ya kuachana ndo utasikia wanachafuana oooh wewe ulikuwa kama gogo na mara ooh wewe ulikuwa kama toothpick mambo kama hayo.
Muonekano
Kuna wakati mtu anapoteza mvuto wake wa asili lakini inakuwa vigumu kwa wapenzi kuambiana ukweli labda mtu amenenepa sana, au amekuwa na kitambi sana na hana mvuto lakini sababu ya mapenzi au uoga inakuwa vigumu wapenzi hawa kuambiana ukweli
Matumizi ya Kilevi
Kwenye matumizi ya pombe baadhi huwa wanakuwa wawazi, lakini wapo wanaoficha matumizi mengine ya kilevi kama kuvuta sigara na matumizi ya miraa au mirungi,
Hisia zake kwa mpenzi wa zamani (EX)
Wapo watu wanaingia kwenye mahusiano wakiwa bado wana hisia za mapenzi na wapenzi wao wa zamani lakini sio rahisi kusema hayo kwa wapenzi wao,na hata wakiulizwa huwa wanadanganya. Na sio raisi kuleta habari za mapenzi ya nyuma kwa mpenzi mpya. Ni vigumu kukwambia anavyojisikia jua ya mpenzi wake wa zamani.
No comments:
Post a Comment