Joh Makini anaamini kumfananisha na rappers wengine ni kutengeneza chuki. Joh Makini amesema hapendi kabisa
kufananishwa na rapper wengine kwasabu hivyo vitu havijengi, vinabomoa
“Sipendi kwasababu mimi tangu naanza mziki wangu nacheza
kwenye level zangu… kama unanifatilia utagundua nna njia yangu kabisa
napita mwenyewe, sio kitu kibaya watu kukufananisha kwasababu wote
tunafanya hiphop na vitu kama hivyo, wakati mwingine unajua hivi vitu
vinazua hata chuki nawatu kutengeneza picha ambazo ni tofauti , na wewe
unaweza kuwa shaidi sisi kama weusi hujawahi kutusikia tukimuongelea
msanii yoyote tofauti au kutengeneza, tunajaribu sana kukwepa hivyo vitu
kwasababu tushagundua havijengi Industry vinabomoa, Kwahiyo sisi
tunalenga sana kwenye kujenga na lengo letu kubwa ni kuendelea kuibrand
hiphop ya Tanzania kwenda kwenye level nyingine kibiashara”
Joh Makini alielezea.
Joh Makini anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Don’t bother aliomshirikisha rapper Aka.
No comments:
Post a Comment